Mtakatifu Simeon alizaliwa kati ya mwaka 390, Kozan (Uturuki sasa).Akiwa na miaka 13 tu, alianza kuchunga kondoo nyikani. Akiwa na miaka 18, siku moja alishindwa kuwapeleka malishoni kondoo, hivyo aliamua kwenda kanisani. Baada ya kumsikiliza mhubiri, aliamua kujiunga na Manosteri iliyokuwa nje ya mjini, iliyoongozwa na Abba John.
Huko alipokelewa na kuanza maisha ya utawa, na baadae mtakatifu Simeon aliomba kupanda na kukaa juu ya mnara uliokuwa hapo katika manosteri, akifunga na kusali.
Mtakatifu Simeon alikuwa na kipaji cha uponyaji, na umaarufu wake ukasambaa kila mahali. Watu walijazana mnarani, kutoka sehemu mbalimbali, wakiombewa. Akajengewa mnara mwingine wa futi 40, ambako alikaa kwa muda mrefu. Kuna wakati Askofu wa Antiokia, alifika hapo, na kumwamuru mtakatifu Simeon kushuka.Alitii nakushuka .Alipewa daraja la ushemasi na kuendelea kukaa mnarani.
Mtakatifu Simeon alikufa akiwa na miaka 75, huko Qalaat Semaan, Byzantine (kati ya Aleppo na Antiokia )
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Apollinaris Syncletica
Mt. Cera
Mt. Charles of Sezze
Mt. Convoyon
Mt. Emiliana
Mt. Gaudentius
Mt. Genoveva Torres Morales
Mt. Gerlac
M/h. Jacques Ledoyen
Mt. John Nepomucene Neumann
Mt. Lomer
M/h. Marcelina Darowska
Mashahidi wa Misri
Mt. Paula
Mt. Roger
Mt. Syncletica wa Alexandria
Mt. Talida
Mtakatifu Simeon, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee....