Mtakatifu Peter Fourier alizaliwa tarehe 30 Novemba 1565 katika kijiji cha Mirecourt, Lorraine , katika himaya ya kirumi (Sasa Ufaransa).Alikuwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto 3.Baba yake alikuwa mchuuzi wa nguo na walikuwa wakristu wakatoliki waaminifu
Akiwa na miaka 15 , baba yake alimwandikisha katika chuo kikuu cha Wa Jesuit , huko Pont-a-Mousson.
Mwaka 1585 Mtakatifu Peter Fourier aliingia katika utawa huko Chaumousey , ambako aliweka nadhiri za mwanzo miaka miwili baadae. Mwaka 1589, Februari 24 alipata daraja la upadri huko Treves.
Wakuu wake walimrudisha tena chuoni (Pont-a-Mousson) kwa masomo zaidi. Huko alisoma zaidi teolojia, akabobea na kupata heshima kubwa chuoni hapo na pia kwa Askofu wa Jimbo la Metz.
Mtakatifu Peter Fourier aliamua kurudi katika kituo chake cha awali.Huko alikumbana na changamoto nyingi kutoka kwa wenzie, akazipokea changamoto hizo kwa moyo mkunjufu. Akapangiwa kufanya kazi katika parokia ya Mattaincourt ambako alifanya kazi kwa miaka 20.
Hapo alifanya mambo makuu mawili.Kwanza aliinua hali ya maisha ya wakazi wa pale kwa kuanzisha benki ambayo haikutoza riba kwa waliokopa. Pili alianzisha mtindo wa mahubiri ambao uliruhusu mdahalo, na maswali katika mambo ya kiimani katika kukuza imani za waamini wake. Alitumia muda mwingi mchana kwa ajiri ya wagonjwa na wahitaji, na usiku aliutumia kwa kusali.
Mwaka 1597 mtakatifu Peter Fourier akishirikiana na mwenyeheri Alix Le Clerc walianzisha shirika lililoitwa Congregation of Notre Dame of Canonesses Regular of st Augustine, ambapo waliapa kusaidia elimu bure kwa watoto .
Katika kipindi kifupi walikuwa tayari wakiendesha shule 6. Shule zilikuwa na taratibu nzuri, kielimu na kimaadili
Mwaka 1621 Askofu wa Toul , Jean des Porcellets , alimuomba kuanzisha jumuia katika jimbo lake. Huko akaanzisha shirika lililoitwa Congregation of our savior , na mwaka 1632 alichaguliwa mkuu wa shirika. Mwaka huo wa 1632 kulitokea uvamizi wa kijeshi mjini wao ukaenda kuwa chini ya utawala wa mfalme Louis XIII wa Ufaransa. Mtakatifu Peter Fourier alikataa kula kiapo cha utii kwa mfalme huyo. Hivyo yeye na wenzake walifukuzwa katika mji huo mwaka 1636. Walienda katika mji jirani wa Gray ambapo pia walifanya kazi nyingi za jamii.
Mtakatifu Peter Fourier alikufa mwaka 1640, Desemba 9.Alitangazwa mwenyeheri mwaka 1730 na papa Benedict XIII na akatangazwa mtakatifu mwaka 1897 na papa Leo XIII..
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Juan Diego
Mt. Balda
Mt. Budoc
Mt. Cyprian
Mt. Ethelgiva
Mt. Gorgonia
Mt. Julian wa Apamea
Mt. Leocadia
Mashahidi wa Samosata
Mashahidi wa Saragossa
Mt. Peter
Mt. Proculus wa Verona
Mt. Restitutus
Mt. Valeria wa Limoges.
Mtakatifu Peter Fourier, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee.....