Mtakatifu Peter Canisius alizaliwa tarehe 8 May 1521, huko Nijmegen, Uholanzi.Baba yake aliitwa Jacob Kanis na mama yake aliitwa Egidia van Houweningen.Mama yake alikufa mara baada ya kumzaa mtakatifu Peter.
Mtakatifu Peter alipelekwa kusoma katika chuo Kikuu cha Cologne , ambako alipata shahada ya uzamili akiwa na miaka 19 tu.Huko chuoni alikutana na Peter Faber ,ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi wa shirika la Wa Jesuit. Hivyo basi ,mwaka 1543 mtakatifu Peter alijiunga na shirika la Wajesuit.
Kupitia mahubiri yake,na maandiko yake, mtakatifu Peter alipata umaarufu mkubwa.Alisafiri toka chuo kimoja kwenda kingine, akifundisha,na kuhubiri.Alipata pia vikwazo mbalimbali katika safari hizo.
Mwana wa mfalme Ferdinand I aliyeitwa Maximilian alimteua Phauser katika baraza lake.Mtakatifu Peter alimuonya mfalme kwa hilo, kwa kuwa Phauser alikuwa akifuata mafundisho ya waprotestanti.Maximilian alitengua uteuzi huo,hali iliyomfanya Phauser,kumchukia mtakatifu Peter kwa kiwango kikubwa.
Mwaka 1547 aliudhuria mabaraza kadhaa, ambako alionekana mahiri katika katekisimu ya kijerumani, ambayo iliwafanya Wajerumani kuelewa mafundisho kwa wepesi.
Akatakiwa kuwa Askofu wa Vienna, lakini alikataa, kwa kuwa alipenda zaidi kuzunguka, akihubiri na kufundisha.Lakini alifanya kazi za utawala katika jimbo mpaka Askofu alipachaguliwa.Akaamia Ujerumani ambako alikuwa mmoja kati ya wataalamu wachache wa Teolojia katika chuo cha Worms mwaka 1557.
Akawa mhubiri mkuu katika cathedral ya Augsburg toka mwaka 1559-1568. Mwaka 1562 alianzisha chuo Kikuu cha Innsbruck.
Alipoamua kuondoka Ujerumani, aliacha shirika la Wa Jesuit likiwa na nguvu na ma Padre wa kutosha.Akaenda Fribourg , Switzerland, ambako alianzisha shule ya matayarisho ya Wa Jesuit nachuo cha mtakatifu Michael, ambacho kiliwaandaa vijana kwa kazi na masomo katika vyuo vikuu.
Mwaka 1591 akiwa na miaka 70, alipata kiharusi, ambacho kilimuacha akiwa amepooza.Lakini aliendelea kuhubiri na kuandika kutumia wasaidizi.
Mtakatifu Peter Canisius alikufa tare he 21 Desemba 1597 huko Fribourg, Switzerland. Akatangazwa mwenye heri mwaka 1864 na Papa Pius IX na akatangazwa mtakatifu mwaka 1925 May 21 na Papa Pius XI.
Watakatifu Wengine wa leo ni
M/h. Adrian
Mt. Anastasius XII
Mt. Andrew Dung Lac
Mt. Glycerius
Mt. Honoratus wa Toulouse
Wt. John na Festus
Mt. John Vincent
M/h. Peter Friedhofen
Mt. Severinus
Mt. Themistoeles
Mtakatifu Peter, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...