Mtakatifu Margaret alizaliwa mwaka 1242 Januari 27, huko Klis, Croatia.Alikiwa binti wa mfalme Bela IV na malkia Mary Lascaris wa Hungaria. Familia yake ilikimbilia Croatia, alipozaliwa, kwa kukimbia uvamizi wa wa Mongolia. Na baba yake aliweka nadhiri kuwa ,wa Mongolia wakiondoka katika nchi yake, basi atamtoa binti yake awe mtawa, amtumikie Mungu.
Mtakatifu Margaret, alikabidhiwa kwa watawa wa Dominican akiwa na miaka 3 tu , katika conventi ya Vesprim. Huko alipata elimu, pamoja na kumjua Mungu.
Akiwa na miaka 12, baba yake alijenga conventi katika kisiwa cha Danube, na hapo akatangaza nia ya kuweka nadhiri zake za mwanzo. Tokea wakati huo, aliishi maisha ya utawa, kama watawa wengine, bila kujali cheo cha familia yake. Alikuwa na kawaida ya kukesha akisali, mbele ya Ekaristi Takatifu kila siku. Mtakatifu Margaret alikufa mwaka 1271 Januari 18, huko Nyulak Szigete,Hungari. Akatangazwa mwenye heri mwaka 1789 Julai 28 na Papa Pius VI .Mwaka 1943 ,November 19 alitangazwa mtakatifu na Papa Pius XII.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Volusian
Mt. Ammonius
Mt. Archelais na wenzake
Mt. Bastmus
Mt. Day
Mt. Deicola
Mt. Fazzio
Mt. Jaime Hilario Barbel
Mt. Leobard
Mt. Liberata
M/h. Marie de la Dive du Verdier
M/h. Monique Pichery
Wt. Moseus na Ammonius
Mt. Ulfrid
M/h. Victoire Gusteau
Mt. Vincenza Mary Lopez y Vicuna
Mtakatifu Margaret, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wa Leo, Mtuombee...