Mtakatifu Lucia , alizaliwa mwaka 283 huko Syracuse Italia.Baba yake alikuwa mkatoliki, lakini alikufa wakati Lucia akiwa na miaka 5 tu.
Katika mji jirani wa Catania,kilometa 50 kutoka Syracuse, kulikuwa na kaburi na kituo cha hija cha mtakatifu Agatha.Mama yake Lucia, Eutychia, alikuwa akienda kusali mahali hapo ,pamoja na mwanae.
Kuna wakati mama Eutychia aliugua mno.Lucie akapata maono kutoka kwa mtakatifu Agatha kuwa mama yake angeponywa.Na muujiza huo ukatokea na akaponywa. Mtakatifu Lucia aliona kuwa ni nafasi nzuri kwake, kumshawishi mama yake ili wagawe baadhi ya vitu vyao kwa maskini.
Baada ya kugawa vitu, gavana wa Syracuse aliyeitwa Paschasius, alifahamu kuwa Lucia na mama yake, walitoa zawadi kwa ajiri ya kumshukuru Mungu. Paschasius alichukizwa na hilo, na akamuamuru Lucia kutoa sadaka ya kuteketezwa mbele ya sanamu ya mfalme. Lucia alikataa . Paschasius aliamuru atupwe jela.
Mtakatifu Lucia alipitia mateso makubwa , ikiwa ni pamoja na kutolewa macho.
Mtakatifu Lucia aliuwawa kwa kukatwa kichwa mwaka 304 huko Syracuse, Italia.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Autbert
Wt. Einhildis na Roswinda
Mt. Elizabeth Rose
Mt. Jodoc
Mtakatifu Lucia, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee....