Mtakatifu John alizaliwa mwaka 1542 huko Fontiveros, Avila, Hispania. Akaitwa Juan de Yepes y Alves.
Baba yake alikufa wakati Mtakatifu John akiwa na miaka 3.Mtakatifu John alipelekwa kusoma katika shule ya maskini na yatima. Huko walifundishwa masomo mbalimbali ,pamoja na dini. Na katika nyakati hizo, alifanya kazi katika manosteri ya mtakatifu Augustinian na katika hospitali.
Mwaka 1563 alijiunga na shirika la Wa Carmelite, ambako alichukua jina la John .Akaweka nadhiri zake mwaka 1564 na akapelekwa kusoma katika chuo kikuu cha Salamanca. Huko alisoma teolojia na filosofia. Na akawa mahili pia katika maandiko matakatifu.
Mwaka 1567, alipata daraja la upadri ,na mwaka 1568 November 28, mtakatifu Theresa wa Avila alianzisha manosteri nyingine. Mtakatifu John, akapendezwa na mipangilio na masharti yake, akajiunga naye, akachukua jina la John wa Msalaba.
Mwaka 1572 alienda Avila kwa mwaliko wa mtakatifu Theresa ambaye alitaka awe mshauri wake wa kiroho. Alikaa huko mpaka mwaka 1577.
Mwaka 1577 kulitokea kutoelewana baina ya wana shirika, na Mtakatifu John alitakiwa aende katika nyumba kuu ya shirika huko Toledo. Lakini aliamua kumtii balozi wa Papa ,ambaye alimtaka akae Avila. Desemba 2 1577, kikundi cha watawa wa Carmelite, walimchukua kwa nguvu mpaka Toledo, ambako alishtakiwa kwa kutokuwa mtii.
Alifungwa hapo Toledo, akipewa adhabu mbalimbali.Alisoma Biblia, na kuandika mashairi .Miezi 9 baadae alitoroka na kujiunga na watawa wa mtakatifu Theresa huko Toledo.Lakini kutokana na kudhoofika kwa afya yake alilazwa hospitali wiki 6.
Mwaka 1579 alitumwa katika mji wa Baeza kuwa mkuu wa chuo kipya cha shirika . Mtakatifu John alitumwa sehemu mbalimbali kuanzisha manosteri mpya za shirika.
Mwaka 1591 mtakatifu John aliugua ugonjwa wa ngozi, ambao ulimletea athari kubwa. Mtakatifu John alikufa mwaka 1591 Desemba 14 ,huko Ubeda, Jaen, Hispania.
Alitangazwa mwenye heri mwaka 1675 januari 25 na Papa Clement X, na akatangazwa mtakatifu mwaka 1726 na Papa Benedict XIII.
Watakatifu Wengine wa leo ni
Mt. Agnellus
Mt. Bartholomew Buonpedoni
Mt. Drusus
Mt. Fingar
Mt. Heron
Mt. Jucundus
Wt. Justus na Abundius
Mt. Matronian
Mt. Nicasius wa Reims
Mt. Nimatullah al-Hardini
Mt. Pompeius wa Pavia
Mt. Spyridon wa Tremithius
Mt. Venantius Fortunatus
Mt. Viator
Mtakatifu John Wa Msalaba, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...