Mtakatifu John, alizaliwa huko Kety, Oswiecim,Poland , mwaka 1390,June 23. Alikuwa mtoto wa Stanislaw na Anna Kanty.
Alisoma katika chuo kikuu cha Krakow ambapo alipata shahada na mwaka 1418,alipata shahada ya udaktari wa filosofia.
Baada ya hapo, alianza kufundisha filosofia katika vyuo Vikuu mbalimbali hadi mwaka 1421 , alipopata daraja la upadri.
Mtakatifu John, akawa mkuu wa chuo cha sheria za kanisa huko Miechow. Alijiendeleza kielimu, akapata tena shahada ya udaktari wa teolojia, na mwisho akawa Profesa.
Katika nyakati hizo, mtakatifu John akawa maarufu katika mji wa Krakow.Alisaidia maskini,na kutenga muda wa kuongea na watu mbali mbali, bila kujali hadhi na vyeo vyao.Akawatafutia wahitaji chakula na nguo.
Mtakatifu John alikufa mwaka 1473 Desemba 24, huko Krakow, Poland. Akatangazwa mwenye heri mwaka 1676 March 28 na Papa Clement X. Akatangazwa mtakatifu mwaka 1767 na Papa Clement XIII
Watakatifu Wengine wa leo ni
Mt. Dagobert II
Mashahidi wa Crete
Wt. Migdonius na Mardonius
Mt. Nicholas Factor
Mt. Servulus
Mt. Theodulus
Mt. Victoria
Mt. Vintila
Mtakatifu John, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...