Mtakatifu John Bosco, alizaliwa mwaka 1815 August 16, huko Becchi , Italia. Baba yake alikufa wakati Mtakatifu John Bosco akiwa na miaka 2.Hivyo yeye na nduguze wawili, walilelewa na mama yao aliyeitwa Margherita. Akiwa na miaka 9 , alianza kuonyesha mwelekeo tofauti na nduguze.Alifanya kazi za shamba, akachunga, na kuhudhuria ibada apasavyo.
Akiwa na miaka 12 alienda kutafuta kazi, ili aweze kujilipia ada ya shule, akiwa na nia ya kusoma na kuwa Padre. Miaka 2 baadae , alikutana na Padre Joseph Cafasso, ambaye aliamua kumsaidia. Mwaka 1835, alijiunga na seminari na mwaka 1841 alipata daraja la upadre. Akapangiwa kufanya kazi katika mji wa Turin, ambao kwa muda huo ulikuwa na vijana wengi,wasio na elimu wala kazi. Alipotembelea gereza, Padre Bosco, alikuta vijana wengi, wenye umri kati ya miaka 12-18. Akasikitishwa mno na hali zao magerezani. Akaamua kufanya jambo ili kuepusha vijana kuingia katika makundi mabaya.
Akaanza kutenga muda wa kuongea nao , kuwafundisha neno la Mungu na kuwatafutia cha kufanya .Mpaka mwaka 1860,kwa msaada wa mama yake, mtakatifu John Bosco alikuwa amewapatia makazi vijana zaidi ya 800.Aliwasaidia pia kupata mikataba mizuri katika kazi, na kati yao alipata vijana wazuri , ambao walikuja kuwa mapadre. Mwaka 1859, alianzisha jumuia ya mtakatifu Francis wa Sale.Akapata waseminari 15 ambao walifanya kazi kwa kujitolea, kufundisha vijana. Mtakatifu John Bosco alikufa mwaka 1888 Januari 31.Akatangazwa Mwenyeheri mwaka 1929 na mwaka 1934 katika sikukuu ya Pasaka , akatangazwa mtakatifu.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Adamnan wa Coldingham
Mt. Aidan wa Ferns
Mt. Athanasius
Mt. Bobinus
Mt. Cyrus
Mt. Domitius
Mt. Eusebius
Mt. Francis Xavier Bianchi
Mt. Geminian
Mt. Julius wa Novara
Mt. Madoes
Mt. Marcella
Mt. Martin Manuel
Mt. Metranus
Mt. Nicetas
Wt. Saturninus, Thrysus, na Victor
Mt. Tarskius
Mt. Trypbaena
Mt. Ulphia
Mtakatifu John Bosco, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...