Mtakatifu Jane Francisca de Chantal alizaliwa Dijon, Ufaransa, 28 Januari, 1572 Baba yake alikuwa rais wa Bunge la Burgundy, na kiongozi wa chama cha kisiasa. Mnamo 1592 aliolewa na Baron de Chantal, na wakaishi katika mji Bourbilly.
Mtakatifu Jane aliishi maisha ya kumcha Mungu , yaliyoleta utulivu katika familia yake na kurudisha ustawi na taratibu nzuri zilizopendeza.
Mumewe, Baron de Chantal aliuawa kwa bahati mbaya na Mtakatifu Jane aliachwa mjane wa miaka ishirini na nane, akiwa na watoto wanne Na hapo aliweka nadhiri ya maisha ya usafi. Katika sala zake zote
alimuomba Mungu ampe mwongozo wa maisha yake.
Mwaka 1604 katika kipindi cha Kwaresma alienda kumtembelea baba yake huko Dijon na akabahatika kumkuta Mtakatifu Francis wa Sale akihubiri. Akatambua mara moja kuwa huyo ndiye msimamizi wake wa kiroho aliyepewa na Mungu. Tokea wakati huo alimwandikia barua nyingi akiomba ushauri katika mambo mbalimbali ya kiroho.
Alitoka mji wa Dijon na kwenda mji wa Annecy kwa ajili ya kuanzisha na kufungua nyumba ya watawa.Tarehe 6 Juni 1610 alifanikiwa kufungua nyumba hiyo.Aliwapokea pia wasichana na wajane na kuwaedeleza njia njema za maisha na kumcha Mungu .Mpaka mwaka 1622 tayari kulikuwa na nyumba 13.Na mwaka alipokufa aliacha nyumba 86 .
Mtakatifu Jane Francisca de Chantal alikufa mwaka
1641 Desemba 13 katika conventi ya Mouli. Mwaka 1751 alitangazwa mwenyeheri na mwaka 1767 alitangazwa Mtakatifu.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mama yetu wa Guadalupe
Mt. Abra
Mt. Agatha
Mt. Alexander
Mt. Amoniria
Mt. Colman wa Glendalough
Mt. Columba wa Terryglass
Mt. Corentin
Mt. Corentius
Mt. Edburga
Mt. Finian wa Clonard
Mt. Hermogenes
Mt. Maxentius
M/h.Thomas Holland
Mt. Vicelin
Mtakatifu Jane, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo , Mtuombee....