Mtakatifu Hilary alizaliwa mwaka 310 huko Pictavium, Gaul. (Ufaransa ) Wazazi wake walikuwa wapagani.
Mtakatifu Hilary alisoma katika shule za kipagani, ambapo alisoma Kigiriki na masomo mengine. Baadae alisoma maandiko matakatifu, na baada ya kuelewa akaamua kubatizwa na kuwa mkristo. Mwaka 350 alichaguliwa kuwa Askofu wa Poitiers.Wakati huo mafundisho ya wapinga Kristo yalikuwa mengi . Mtakatifu Hilary alianza kupambana na watoa mafundisho ya uongo.Akaandika nyaraka mbalimbali kwa mfalme Consantius, pamoja na majimbo kadhaa kupinga mafundisho na madhulumu kwa wakristo. Kutokana na hayo , mtakatifu Hilary alipelekwa uhamishoni huko Phrygia (Uturuki sasa ) ambako alikaa miaka 4 .Akiwa huko aliendelea kuongoza jimbo lake, akaandika barua mbili za mafundisho ambazo zilisambazwa katika miji mbalimbali. Mtakatifu Hilary alirudi jimboni mwake mwaka 361.Akaendelea kuandika machapisho mbalimbali ya mafundisho. Mtakatifu Hilary alikufa mwaka 367, huko Poitiers, Gaul.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Agrecius
Mt. Andrew wa Trier
Mt. Berno wa Cluny
Mt. Elian
Mt. Erbin
Mt. Enogatus
Mt. Erbin wa Dumnonia
Mt. Glaphyra
Mt. Gumesindus
Mt. Hermylus
Mt. Kentigern Mungo
Mt. Leontius wa Caesarea
Mt. Viventius
M/h. Yvette
Mtakatifu Hilary, Wenyeheri Na Watakatifu Eengine Wa Leo, Mtuombee....