Mtakatifu Gildas, inakadiriwa kuwa alizaliwa mwaka 517,kaskazini mwa Uingereza. Alizaliwa katika familia yenye hadhi kubwa.Alipata elimu njema, na alikuwa pia mcha Mungu. Aliamua kwenda kuishi peke yake, akisali na kuomba, katika kisiwa cha Flatholm. Alienda pia katika sehemu tofauti, akihubiri.
Mwaka 547, aliandika vitabu mbalimbali vyenye mafundisho .Baadae akaenda katika mji wa Rhuys katika Uingereza, ambako alianzisha monasteri, na yeye akiwa Abate wa monasteri hiyo. Mtakatifu Gildas alikufa mwaka 571, katika monasteri ya Rhuys.Anakumbukwa kama moja ya nguzo imara katika Kanisa, nchini Uingereza.
Watakatifu wengine wa leo ni
Wt. Sarbelius na Barbea
Mt. Aquilinus
Mt. Blath
M/h. Boleslava Lament
Mt. Caesarius
Mt. Dallan
Wt. Papias na Maurinus
Mt. Sabinian wa Troyes
Mt. Valerius wa Troves
Mt. Voloc
Mtakatifu Gildas, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...