Mtakatifu Francisca, alizaliwa mwaka 1850, Julai 15, huko Lombard, wakati huo chini ya ufalme wa Austria. Baba yake aliitwa Agostino Cabrini na mama Stella Oldini.
Akiwa na miaka 13 alianza shule ambayo iliendeshwa na watawa (masista).Miaka 5 baadae, alihitimu shahada ya ualimu. Mwaka 1870, aliomba kujiunga na shirika la watawa (Daughters of the Sacred Heart ) ambao walimkatalia kutokana na kuwa na afya mbaya.Akawa mkuu wa shule ya watoto yatima katika mji wa Codogno.
Hapo Codogno ,alianzisha jumuia ya wanawake,ambao waliamua kumtumikia Mungu na mwaka 1877,waliweka nadhiri za mwanzo.Naye akaongeza jina la Xavier, kwa heshima ya Mt Francis Xavier.
Mwaka 1880, mtakatifu Francesca na wenzake sita, walianzisha shirika la watawa (Missionary Sisters of the Sacred Heart of Jesus ).Kazi yao kubwa ikawa ni kufungua shule kusaidia watoto yatima kusoma bila gharama.
Mwaka 1877, Mtakatifu Francesca aliomba kibali cha Papa kufanya utume wake huko China.Lakini akashauriwa kuanzia Marekani kwanza, ambako kulikuwa na wahamiaji wengi kutoka Italia, ambao walikuwa maskini.
Aliondoka kwenda Marekani na akafika New York mwaka 1889, March 31, akifuatana na watawa 6.
Japo alipata vikwazo vingi, mtakatifu Frances aliweza kuanzisha shule, akifundisha katekisimu na masomo ya kawaida. Afanikiwa kuanzisha shule nyingi na mahospitali katika Marekani yote.Na baadhi ya watawa wa shirika lake walienda China.Naye akawa raia wa Marekani.
Mtakatifu Francisca Xavier Cabrini alikufa mwaka 1917 Desemba 22 huko Chicago Illinois, Marekani.Alitangazwa Mwenyeheri mwaka 1938 November 13 na Papa Pius XI, na akatangazwa mtakatifu mwaka 1946 Julai 7 ,na Papa Pius XII.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Chaeromon
Mt. Amaswinthus
Mt. Demetrius
Mt. Flavian
Mt. Hunger
Mt. Zeno
Mtakatifu Francisca, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo,Mtuombee....