Mtakatifu Francis wa Sale alizaliwa tarehe 21 August 1567, huko Savoy Ufaransa. Alizaliwa katika familia iliyoheshimika, baba yake aliitwa François de Sales na mama yake François de Sionnaz.
Alibatizwa jina la Francis Bonaventure. Alianza masomo yake La Roche-sur-Foron, na baadae katika shule ya wa Capuchin huko Annecy.
Mwaka 1583 alijiunga na chuo cha Clermont mjini Paris, na kisha katika chuo cha Wa Jesuit. Aliambatana na mtumishi wake.
Mwaka 1588 , alimaliza masomo yake hapo Clermont, na akajiunga na chuo kikuu cha Padua Italia. Hapo alisoma teolojia na sheria. Mwaka 1592 alipata shahada ya udaktari wa sheria na teolojia. Baada ya hapo, baba yake alimtafutia kazi nzuri na mchumba , lakini mtakatifu Francis alikuwa na mwelekeo tofauti , aliamua kumtumikia Mungu. Na mwaka 1593, alipata daraja la upadri na akaanza kufanya kazi katika Cathedral ya Geneva. Alipata upinzani kutoka kwa wapinga Kristo katika mji wa Chablais, na kulifanyika majaribio kadhaa ya kumuua,bila mafanikio. Mwaka 1602 Askofu Granier wa Geneva alikufa.
Mtakatifu Francis akasimikwa kuwa Askofu wa Geneva.Akiwa Askofu, akihubiri na kufundisha, akiandika vitabu na nyaraka mbalimbali. Mtakatifu Francis wa Sale alikufa mwaka 1622 December 22, baada ya kuugua kiharusi. Alitangazwa mwenye heri mwaka 1661 na Papa Alexander VII na miaka minne baadae akatangazwa mtakatifu na Papa Alexander VII. Mwaka 1877 alitangazwa kuwa Daktari wa Kanisa na Papa Pius IX
Watakatifu wengine wa leo ni
M/h. Anicet Hryciuk
Mt. Artemius
Mt. Babylas
M/h. Bartlomiej Osypiuk
Mt. Bertrand
M/h. Daniel Karmasz
Mt. Exuperantius wa Cingoli
Mt. Felician wa Foligno
M/h. Filip Geryluk
Mt. Guasacht
M/h. Ignacy Franczuk
M/h. John Grove
Mt. Macedonius
Mt. Mardonius
Mt. Messalina
M/h. Michal Wawryszuk
M/h. Onufry Wasyluk
Wt. Thyrsus na Projectus
M/h. William Ireland
Mt. Zama
Mtakatifu Francis, Wenye Heri na Watakatifu Wengine Wote wMWa Leo, Mtuombee...