Mtakatifu Elizabeth alizaliwa mwaka 1774 August 28 huko New York city. Mwaka 1794 aliolewa na William Magee Seton ambaye alikuwa mfanyabiashara.
Mume wake (William Seton )alifariki mwaka 1803, huko Italia. Na Mtakatifu Elizabeth alipoenda huko, ndipo alipoamua kuwa mkatoliki.
Mtakatifu Elizabeth alirudi Marekani mwaka 1805, na kuanza maisha mapya, akiwa mjane, mkatoliki. Na mwaka 1809 aliamia Emmitsburg, Maryland ambako alianzisha shirika (Charity of Saint Joseph ), ambalo lilikuwa la kwanza kwa watawa wanawake nchini Marekani.
Alianzisha pia shule (St Joseph academic )ambayo walisomesha watoto maskini bure.Shule hiyo ikawa chachu kwa elimu katika jamii za wakatoliki, na kusaidia wasioweza kumudu gharama za shule.
Mtakatifu Elizabeth Ann Seton alikufa mwaka 1821, Januari 4 huko Emmitsburg, Maryland Marekani.
Alitangazwa mwenye heri mwaka 1963 March 17 na Papa John XXIII, na akatangazwa mtakatifu mwaka 1975 Sept 14 ,na Papa Paul VI.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Abraham
M/h. Angela wa Foligno
Mt. Aquilinus
Mt. Dafrosa
Mt. Eugendus
Mt. Ferreolus wa Uzes
Mt. Hermes
Mt. Libentius
M/h. Manuel Gonzalez Garcia
Mt. Mavilus
Mt. Pharaildis
Mt. Rigobert (Robert)
M/h. Thomas Plumtree
Watakatifu Rigobert na Elizabeth, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wa Leo, Mtuombee....