Mtakatifu Damasus, alizaliwa mwaka 305 huko Roma Italia. Baba yake aliitwa Antonius na mama yake aliitwa Laurentia.
Mwaka 354, akiwa shemasi alifuatana na Papa Liberius, ambaye alipelekwa uhamishoni katika mji wa Berea na mfalme Consantius II.
Akiwa huko uhamishoni na Papa, mtakatifu Damasus alimsaidia Papa katika mambo mengi ya uendeshaji wa kanisa.Na mwaka 366 September 24, Papa Liberius alikufa .
Mtakatifu Damasus alichaguliwa kuwa Papa .Lakini alipata upinzani mkubwa kutoka kwa kundi lisilompenda.Lakini mwaka 378 alitibitishwa kuwa Papa.
Mtakatifu Damasus, alikuwa na kazi nyingi za kuleta umoja na maelewano katika kanisa.Akamchagua Mtakatifu Jerome kuwa Katibu wake kwa kazi maalum. Na akampa moyo kufanya kazi ya kutafsiri Biblia kutoka Kigiriki kwenda kilatini.
Mtakatifu Damasus I Papa , alikufa mwaka 384 Desemba 11, huko Roma ,Italia.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Acepsius
Mt. Barsabas
Mt. Cian
Mt. Damasus
Mt. Daniel
Mt. Eutychius
Mt. Fidweten
M/h. Martin
M/h. Melchiorof
Mt. Pens
Mt. Sabinus
Mt. Trason
Wt.Victoricus,Fuscian,na Gentian
Mtakatifu Damasus I, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...