Mtakatifu Caesarius alizaliwa kati ya mwaka 470 huko Chalon-sur-Saône ,Ufaransa. Akiwa bado kijana, alijiunga na monasteri ya Lerins.
Alikuwa na bidii katika kazi zote alizopangiwa, na kusali pamoja na kufanya majitoleo mbalimbali.Akapata tatizo la afya yake na hiyo ikasababisha kuhamishwa kwenda Arles.
Akiwa Arles akaendelea na mwenendo mwema, akipita katika kazi mbalimbali na mwisho kutangazwa Askofu wa Arles.
Mtakatifu Caesarius akiwa askofu, aliendelea kuimarisha ukristo katika Gaul (Ufaransa ) akisisitiza katika mafundisho ya kweli, na akihimiza wanadamu kumrudia Mungu. Mtakatifu Caesarius alikufa katika mwaka 542, huko Arles, Ufaransa.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Marguerite Bourgeoys
Mt. Aelred wa Rievaulx
Mt. Anthony Mary Pucci
Mt. Arcadius
Mt. Bartholomew Alvarez
Mt. Benedict Biscop
Mt. Caesaria
M/h. John Gaspard Cratz
Mt. John wa Ravenna
Mt. Margaret Bourgeoys
Mt. Martina
Mt. Martin wa Leon
Mashahidi wa Ephesus
M/h. Pierre-Francois Jamet
Mt. Salvius
Mt. Tatiana wa Rome
Wt. Tigrius na Eutropius
Mt. Victorian
Mt. Victorian wa Asan
M/h. Vincent de Cunha
Mt. Zoticus
Mtakatifu Caesarius, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee....