Mtakatifu Brigid Wa Ireland, Mtawa
Mtakatifu Brigida alizaliwa mwaka 451 huko Faughart, Dundalk, Ireland. Baba yake aliitwa Dubthach na mama yake aliitwa Brocca.Mama yake alikuwa mkristo,na baba mpagani.
Mama yake ,aliuzwa kama mtumwa kwa mganga wa kienyeji , na mtakatifu Brigida alilelewa huko.Lakini alirejea kwa Baba yake alipofikisha miaka 10.Alikuwa na tabia ya huruma, akisaidia kila mtu kwa alichoweza kupata. Baba yake Kukupendezwa na tabia hiyo ,hivyo nae alimpeleka kwa mfalme Leinster, kwa lengo la kumuuza. Lakini wakati akiongea na mfalme, mtakatifu Brigida alichukua upanga wa baba yake, wenye thamani, akampa maskini, ili auuze na kununua chakula. Mfalme aliposhuhudia hilo, alimwambia Dubthach kumuacha Brigida huru kwa kuwa aliona kuwa ni mtu ambaye anatenda mema.
Aliporuhusiwa na baba yake kuondoka, alienda kwa mama yake, kumsaidia katika kazi ya kutunza mifugo, akisimamia kuuza maziwa. Lakini napo aliendelea na tabia yake, na japo kwa nyakati,alitoa maziwa bure , lakini biashara ilikuwa na faida kubwa kwa yule mganga wa kienyeji. Kwa kufurahia hilo, mganga alimuachia huru Brocca, ambaye ni mama yake na mtakatifu Brigida. Mtakatifu Brigida alikataa kuolewa, na kujitoa kwa Mungu.Akiwa na miaka 40 alianzisha manosteri ya Kildare. Alianza kwa kuwa na wanawake 7, ambao nao walikuwa na msimamo kama wake , wa kumtumikia Mungu. Mtakatifu Brigida aliendelea kusaidia kwa kila alichoweza, mpaka tarehe 1 Februari mwaka 525, alipokufa.
Watakatifu wengine wa leo ni
M/h. Luigi Variara
M/h. Andrea Carlo Ferrari
M/h. Andrew of Segni
M/h. Anne-Francoise de Villeneuve
M/h. Anne Hmard
M/h. Anthony Manzi
M/h. Catherine Cottenceau
Mt. Cinnia
Mt. Crewanna
Mt. Darulagdach
M/h. Francoise Bonneau
M/h. Francoise Michau
M/h. Francoise Pagis Roulleau
M/h. Gabrielle Androuin
Mt. Jarlath
M/h. Jeanne Bourigault
M/h. Jeanne Fouchard Chalonneau
M/h. Jeanne Gruget Doly
M/h. Jeanne-Marie Sailland d'Epinatz
Mt. John Grating
Mt. Kinnia
M/h. Louise-Aimee Dean de Luigne
M/h. Louise-Aimee Dean de Luigne
M/h. Louise Rallier de la Tertiniere Dean de Luigne
M/h. Luigi Variara
M/h. Madeleine Blond
M/h. Madeleine Cady
M/h. Madeleine Perrotin Rousseau
M/h. Madeleine Sailland d'Epinatz
M/h. Madeleine Salle
M/h. Marguerite Riviere Huau
M/h. Marguerite Robin
M/h. Marie Cassin
M/h. Marie-Genevieve Poulain de la Forestrie
M/h. Marie Grillard
M/h. Marie-Jeanne Chauvigne Rorteau
M/h. Marie Lenee Lepage Varance
M/h. Marie Leroy Brevet
M/h. Marie Pichery Delahaye
M/h. Marie Roualt Bouju
M/h. Marthe Poulain de la Forestrie
Mt. Paul of Trois Chateaux
M/h. Perrine Androuin
M/h. Perrine Besson
M/h. Perrine Bourigault
M/h. Perrine Grille
M/h. Perrine-Jeanne Sailland d'Epinatz
M/h. Perrine Laurent
Mtakatifu Brigid, Watakatifu Na Wenye Heri Wengine Wote Wa Leo , Mtuombee...