Mtakatifu Bibiana, alikuwa Binti wa Flavian, shujaa wa kirumi na mkewe Dafrosa, ambao walikuwa wakristo.
Mwaka 363 , Mtawala wa dola ya kirumi, alimteua Apronianus kuwa gavana wa Roma. Gavana huyo alimkamata Flavian na baada ya mateso makali, alimpeleka uhamishoni, ambako alikufa. Mkewe Dafrosa alikatwa kichwa.
Bibiana na dada yake aliyeitwa Demetria, waliachwa katika umaskini mkubwa.Walikaa na njaa muda mwingi, wakisali na kuomba.Gavana Apronianus aliamuru waletwe mbele yake . Demetria alipoulizwa kuamua imani yake, alikiri imani na kufa hapo hapo.
Bibiana alikabidhiwa kwa mwanamke mmoja aliyeitwa Rufina.Rufina alimtesa mno na kumfanyia mabaya. Lakini hakukata tamaa, na mwisho , Apronianus aliamuru afungwe katika nguzo na kupigwa hadi kufa.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Chromatius
Mt. Eusebius
Mt. Evasius
M/h. Ivan Sleziuk
Mt. Lupus of Verona
M/h. Maria Angela Astorch
Mt. Pontian
Mtakatifu Bibiana, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...