Mtakatifu Berard alizaliwa huko Carbio, Umbria. Mwaka 1219 Mtakatifu Berard na wenzake wa Franciscan , Peter, Adjute, Accurs, Odo na Vitalis, waliondoka kwenda kuhubiri neno la Mungu huko Morocco.
Katika safari hiyo walipitia Hispania. Lakini wakiwa Hispania, mwenzao Vitalis, alipata ugonjwa, uliosababisha yeye kushindwa kuendelea na safari hiyo.
Hivyo aliwaomba wenzake kuendelea na safari hiyo bila yeye. Walipofika katika mji wa Seville, walihubiri, na kuendelea na safari yao kwenda Morocco. Walipofika, walianza kuhubiri sokoni ,ambako kulikuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu.
Wakakamatwa na kupewa amri ya kuondoka Morocco mara moja.Lakini walikataa na wakaendelea kuhubiri.Sultani wa Morocco aliamuru wakamatwe na kuuwawa.Mtakatifu Berard na wenzake walikamatwa, na baada ya mateso na vipigo vikali, walikatwa vichwa na sultan mwenyewe tarehe 16 Januari 1220. Hawa walikuwa ni mashahidi wa kwanza wa Franciscan, na walitangazwa watakatifu mwaka 1481,August 7,na Papa Sixtus IV.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Fursey
Mt. Dunchaid O'Braoin
Wt. Fusca na Marura
Mt. Henry wa Cocket
Mt. Honoratus
Mt. James wa Tarentaise
Mt. Liberata
Mt. Melas
Mt. Titian wa Oderzo
Mt. Triverius
Mt. Valerius
Watakatifu Berard, Peter, Adjute, Accurs Na Odo, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...