Mtakatifu Anysia alizaliwa huko Solanika, Thessaly, Ugiriki, katika familia ya kikristo.
Aliamua kuweka wakfu maisha yake, kuishi maisha safi na ya kimaskini , akisali na kusaidia maskini.
Lakini nyakati hizo zilikuwa nyakati za madhulumu kwa wakristo, chini ya utawala wa mfalme mpagani Maximian ambaye alikuwa Mrumi.
Mwaka 304, alitoka kwenda kanisani, na njiani akakutana na askari wa Kirumi.Askari huyo alipogundua kuwa Anysia ni mkristo, alianza kumpiga na alitaka kumpeleka katika hekalu la kipagani ,amtoe sadaka.
Alipomchania ushungi wake, kwa kumdhalilisha, mtakatifu Anysia alimtemea mate usoni. Askari huyu, alimchoma na upanga, ambao ulitokeza mpaka upande wa pili, na kumuua.
Watakatifu Eengine Wa Leo Ni
Mt. Anysius
Mt. Egwin wa Evesham
Mt. Eugene
M/h. John Alcober
Mt. Liberius wa Ravenna
Mt. Mansuetus
Mt. Raynerius
Mt. Sabinus
Mtakatifu Anysia, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...