Mtakatifu Antony, alizaliwa mwaka 251 ,huko Herakleopolis, Magna, Misri. Wazazi wake walikufa akiwa na miaka 18.
Wazazi walipokufa, aligawa mali zake zote kwa maskini ,na akaamua kuishi maisha ya kitawa , akifanya kazi na kusali, na akaamua kwenda kuishi jangwani. Akaishi miaka mingi jangwani, akipata majaribu kutoka kwa shetani.Mwaka 311 alienda Alexandria kwa ajili ya kuwapa faraja wakristo, ambao walikamatwa na kushtakiwa , kwa amri ya mfalme Maximian.
Mtakatifu Antony, aliendelea na kupambana na wapinga Kristo , na alikufa mwaka 356, huko mlima Colzim , Misri.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Achillas
M/h. Gonzalo de Amarante
M/h. Gregory Khomyshyn
Mt. Julian Sabas
Mt. Mildgytha
Mt. Nennius
Mt. Pior
Mt. Sulpicius
Mtakatifu Anthony, Wenye Heri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee...