Mtakatifu Angela Merici, alizaliwa mwaka 1474 March 21, huko Desenzano, Lombardy - Italia.
Akiwa na miaka 10 , wazazi wake walikufa na akabaki na dada yake tu. Na baada ya muda mfupi, dada yake nae alikufa.
Mtakatifu Angela alijiunga na utawa wa tatu wa mtakatifu Francis, ambako aliweka nadhiri kuishi Bikira. Akiwa na miaka 20, mjomba wake, ambaye ndiye aliyekuwa mlezi wake, alikufa.
Mtakatifu Angela aliamua kurudi kijijini kwao Desenzano, ambako aliona wasichana wengi wakiishi maisha yasiyopendeza.Hawakuwa na elimu wala matumaini.Na wazazi wao hawakujali. Aliamua kufungua kituo nyumbani kwao, akiwafundisha wasichana hao imani ya kanisa Katoliki. Akiwafundisha pia kusali. Mwaka 1524 alifanya hija nchi takatifu, lakini alipata maradhi ya upofu katika kisiwa cha Crete. Aliendelea na hija hiyo akiwa kipofu akipita sehemu zote. Akiwa njiani kurudi nyumbani, aliweza tena kuona.Mwaka 1525 alienda Roma kuhiji, na Papa alisikia habari zake na alimfurahia mno.
Mwaka 1535 November 25, Mtakatifu Angela akiwa na mabikira 12, walianzisha rasmi shirika la watawa (Order of the Ursulines) katika nyumba ndogo ,karibu na kanisa la mtakatifu Afra ,katika mji wa Bresica. Shirika lilikuwa, na kufungua vituo vya yatima na shule.Mwaka 1537 Mtakatifu Angela alichaguliwa kuwa mkuu wa shirika. Na sheria na kanuni za shirika zilipitishwa mwaka 1544 na Papa Paul III. Mtakatifu Angela alikufa mwaka 1540,Januari 27, akazikwa katika kanisa la mtakatifu Afra Bresica. Alitangazwa mwenye heri mwaka 1768 April 30 na Papa Clement XIII. Akatangazwa mtakatifu mwaka 1807 May 24 na Papa Pius VII
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Aviates
Mt. Avitus
Mt. Candida
Mt. Datius
Mt. Devota
Mt. Emerius
Mt. Gamelbert wa Michaelsbuch
Mt. Gamo
Mt. Gilduin
Mt. Henry de Osso y Cervello
Mt. Julian wa Le Mans
Mt. Julian wa Sora
Mt. Lupus wa Chalons
Mt. Marius
Mt. Maurus
Mt. Natalis
M/h. Rosalie du Verdier de la Soriniere
Mt. Sabas wa Serbia
Mt. Theodoric wa Orleans
Mtakatifu Angela, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee