Mtakatifu Andrew alizaliwa katika karne ya kwanza huko Bethsaida, Kando ya ziwe Galilee. Alikuwa mwana wa Jonah, na alikuwa pia ndugu wa Mtakatifu Peter Mtume. Naye pia alikuwa mvuvi (Mt 4:18).
Mtakatifu Andrew alimtambua pia Bwana Yesu kuwa ni Masia (Yn 1:35-40) .Ni yeye pia, aliyetambua uwepo wa mvulana aliyekuwa na chakula kidogo mkutanoni (Yn 4:8-9).
Baada ya kufa,kufufuka na kupaa kwa Bwana, Mtakatifu Andrew aliondoka na kwenda kuitangaza Injili katika miji mbalimbali, katika nchi za Uturuki na Ugiriki.
Mtakatifu Andrew aliuwawa kwa kutundikwa katika msalaba, ambao ulikuwa tofauti na msalaba wa Bwana Yesu Kristo, kati ya mwaka 60 huko Patras , kwa amri ya Nero, aliyekuwa Mtawala wa dola ya Warumi nyakati hizo.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Constantius
Mt. Joseph Marchand
Mt. Maura
Mt. Trojan
Mt. Tudwal
Mtakatifu Andrew, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee.....