Mtakatifu Adrian alizaliwa Afrika ya kaskazini.Akawa Abate wa monasteri ya Nasidanum, iliyokuwa karibu ya Naples.
Alichaguliwa kuwa mara mbili na Papa kuwa Askofu wa Canterbury , lakini alikataa kwa sababu mbalimbali.Lakini mwisho Askofu aliyeteuliwa wa Canterbury, alimteua Mtakatifu Adrian kuwa Abate wa monasteri ya watakatifu Peter na Paul.
Kutokana na uongozi wake thabiti, monasteri iliongeza ufanisi katika elimu, na mambo ya kiimani.
Mtakatifu Adrian Abate, alikufa mwaka 710, na akazikwa katika monasteri ya watakatifu Peter na Paul
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Abhor (Amba Hor)
Mt. Basilissa
Mt. Brithwald
Mt. Epicharis
Mt. Foellan
Mt. Honorius
Wt. Julian na Basilissa
Mt. Marciana wa Mauretania
Mt. Maurontus
Mt. Paschasia
M/h. Tommaso Reggio
Mt. Vitalicus
Mt. Waningus
Mtakatifu Adrian, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee....