_*Leo Kanisa Linakumbuka Kutolewa Kwa Bikira Maria Hekaluni*_
Bikira Maria alizaliwa na baba Joachim na mama Anna.Akiwa na miaka 3 wazazi wake hao , walimtoa hekaluni huko Jerusalem.Bikira Maria alikaa huko hekaluni hadi alipofikisha miaka 12.
Kanisa linakumbuka siku hii tokea mwaka 543, ambapo kulijengwa hekalu kubwa kumuenzi Mama yetu, Bikira Maria.Hekalu hilo lilibomolewa katika vita mwaka 614.Kumbukumbu hiyo iliendelezwa tena katika karne ya 9, na mwaka 1372 Papa Gregory IX aliitambua rasmi.
Mababa wa kanisa katika vipindi mbalimbali waliendelea kuiimarisha kumbukumbu hiyo katika vipindi mbalimbali.Papa Clement VIII aliimarisha zaidi mwaka 1597.Ikaingia katika kalenda ya kanisa mwaka 1969.
Mama Maria, utuombee.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Gelasius
Mt. Albert wa Louvain
Mt. Amelberga
Mt. Digain
Mt. Gelasius I
Mt. Heliodorus
Mt. Hilary
Mt. Honorius
Mt. Liberalis
Bl. Frances Siedliska
Mt. Maurus
Mt. Rufus wa Rome
Mama Yetu Maria, Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa leo, _Mtuombee......🙏