*Kanisa la mtakatifu Petro*
Basilica la mtakatifu Petro na , lilianza kujengwa mwaka 319, na Mfalme Constantine mkuu. Likaisha mwaka 333.
Lakini lilichakaa na kuharibika kutokana na sababu mbalimbali.Mwaka 1447, Papa Nicholas alianza mpango wa kulifanyia ukarabati.
Likaanza kukarabatiwa chini ya wataalamu bora kabisa na pia chini ya ma Papa mbali mbali, katika vipindi tofauti, hadi mwaka 1626 November 18, lililotabarukiwa na Papa Urban VIII.
*Kanisa la Mtakatifu Paulo*
Basilica la mtakatifu Paulo, lilianza kujengwa pia katika karne ya 3.Na kazi hiyo ilianzishwa na mfalme Theodosius na Papa Leo Mkuu.
Mwaka 1823, Basilica hilo, liliteketea kwa moto.Likaanzwa kujengwa upya kwa nguvu, na kuchangiwa na watu wengi, wakatoriki na wasio wakatoliki.
Mwaka 1854, December 10, Basilica jipya la mtakatifu Paulo, lilitabarukiwa na Papa Pius IX.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Rose Philippine Duchesne
Mt. Anselm
M/h. Grimoaldo
Mt. Hesychius wa Antioch
M/h. John Shoun
M/h. Karolina Kozka
Mt. Keverne
Mt. Leonard Kimura
Mt. Mabyn
Mt. Mawes
Mt. Maximus
Mt. Mummolus
Mt. Nazarius
Mt. Odo
Mt. Oriculus na wenzake
Wt. Romanus na Barula
Mt. Thomas wa Antioch
*Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, _Mtuombee.....🙏_*