Sherehe ya Bikira MARIA Mtakatifu Mkingiwa Dhambi ya Asili, ilianza kusheherekewa katika karne ya tano huko Sirya. Na ikaenea katika nchi nyingi kulingana na mapokeo.
Lakini baada ya kupita katika mijadala mbalimbali, mwaka 1854, Papa Pius IX, alitangaza rasmi Desemba 8 kuwa sherehe ya Mama Bikira Maria , kukingiwa dhambi ya asili.Na hilo ni fundisho la kanisa.
Utakatifu wa Maria ni matokeo ya neema ya Mungu na utayari wake wa kuwa wazi kwa neema hiyo. Kutokupata dhambi ya asili ni kwasababu ya neema ya Mungu kupitia kwa Mwanae Bwana wetu Yesu Kristo. Kwahiyo Maria kukingiwa dhambi ya asili sio namna ya kumpa heshima kwa njia yake mwenyewe bali kwa njia ya Mwanae Yesu Kristo. Kristo kutokuwa na dhambi ni kwasababu ya yeye kuwa nafsi ya pili ya Mungu. Na Maria kutokuwa na dhambi ni kwasababu ya neema ya Mungu pekee na kushirikiana kwake na neema hiyo.
Kanisa la kwanza walimheshimu Bikira Maria kwa namna ya pekee kati ya watakatifu wote, kwasababu ya kushiriki kwake katika fumbo la umwilisho wa Mwanae Yesu Kristo na kwa sababu ya neema iliotoka katika kushiriki kwake katika fumbo hili.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Romaric
Mt. Eucharius
Mt. Macarius
Mt. Patapios wa Thebes
Mama Yetu, Bikira Maria, Utuombee Sisi Wakosefu, Sasa Na Saa Ya Kufa Kwetu .
Wenyeheri Na Watakatifu Wengine Wote Wa Leo, Mtuombee.....