Mama Maria ni mama wa Mungu. Mwaka 431 huko Efeso , Katika mtaguso, kulipitishwa azimio la Mama Maria ni Mama wa Mungu (Theotokos). Bikira Maria alimzaa Kristo Yesu ambaye ni Mungu kweli na mtu kweli ni Mama ya Mungu – mtaguso huo wa Efeso ulivyoweka wazi: Bikira Maria ni Mama kweli wa Yesu, kwa kuwa hali ya ubinadamu wa Yesu ilichangiwa na Mama Bikira Maria kwa ukamilifu wote. Pili, Bikira Maria ni kweli Mama wa Mungu, kwa kuwa alichukua mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaa nafsi ya Pili ya Mungu – Mungu Mwana, Mkombozi wetu Yesu Kristo kama tunavyosali katika Kanuni ya Imani; “Nasadiki kwa Bwana Mmoja Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu. Aliyezaliwa kwa Baba, tangu milele yote. Mungu aliyetoka kwa Mungu, mwanga kwa mwanga, Mungu kweli kwa Mungu kweli.
Japo kuwa twasema kuwa hilo ni fundisho la kanisa, lakini pia twaweza kurejea katika maandiko Luka 1:26-38 , Luka 1:42-43, na Pia Wagalatia 4:4.
Pia Baba Mtakatifu Paulo VI mwaka 1968 akaitenga siku hii kuwa pia ni siku ya kuombea amani ulimwenguni maana ujumbe wa Malaika siku ya Noeli ni Amani kwani Mtoto aliyezaliwa ni mfalme wa amani.
More Saints of the Day
Mt. Almachius
Mt. Basil
M/h. Berka Zdislava
Mt. Clarus
Mt. Concordius
Mt. Connat
Mt. Cuan
Wt. Elvan & Mydwyn
Mt. Euphrosyne
Mt. Fanchea
Mt. Fulgentius wa Ruspe
Mt. Giuseppe Maria Tommasi
M/h. Jean-Baptiste Lego
Mt. Joseph Mary Tommasi
Mt. Justin wa Chieti
Mt. Maelrhys
Mt. Magnus
Mt. Odilo
M/h. Rene Lego
Mt. Telemachus
M/h. Valentin Paquay
Mt. William wa Dijon
Mt. Zdislava Lemberk
Mt. Zygmunt Gorazdowski
Maria Mtakatifu Mama Wa Mungu, Utuombee Sisi Wakosefu, Sasa Na Saa Ya Kufa Kwetu , Amina