Karibuni ndugu zangu kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana linazungumzia bado juu ya ujio wa nyakati za mwisho na linazidi kumhimiza mkristo apate kujiandaa vyema Zaidi na Zaidi kwa ujio wa wakati wa mwisho maishani mwake. Katika somo la kwanza, mwandishi wa kitabu cha Daniel anamwakilisha mfalme Antiokus Epihanes IV kama pembe. Pembe hii ilikuwa na macho na mdomo na mdomoni mwake kulitoka maneno ya kiburi na matukano yakiwatunakana watu wa Mungu. Pembe hii iliwapiga sana watu wa Mungu, yaani Wayahudi wa kipindi cha Wamakabayo na ilibahatika kuwaua wengi sana hadi Wayahudi wakakata tamaa na baadhi wakafikiri kwamba hakuna kama hii pembe, hakuna kama huyu Antiokus. Hata Mungu wetu amemshindwa huyu Antiiokus kwa sababu ameshawaua watu wake na yeye hafanyi kitu. Matendo yaliyofanywa na huyu Antiokus yanafanana kabisa na yaliyofanywa na yule limnyama la ajabu katika ufunuo sura ya kumi na tatu ambalo lilimwakilisha Kaisari Nero na ukatili wote aliowafanyia Wakristo wa kanisa la mwanzo.
Lakini Danieliku ya kimaisha kwetu yanakuwa kama huyu Antiokus, yaani tunayaona kwamba yana nguvu ajabu, huwezi kuishi duniani bila hayo, bila hizo anasa au hataweza kutulia bila kuyafikiria. Lakini mwishoni, haya tunayodhania kuwa ndiyo yenyewe, mwishowe tutakuja kuonyeshwa kwamba hayana nafasi yoyote, vile kama Antiokus anavyoonyeshwa leo kwamba japokuwa anaonekana kama vile ana nguvu Zaidi ya kila kitu, kumbe ni bure tu.
Kwa tafakari hiyo, tunaalikwa kuchunguza nguvu za kila kinachotutishia, je, hiki kitu kinachotufanya tusilale usingiizi kina nguvu kiasi gani? Uwezo wake wa kutishia ni mkubwa kiasi gani, kanaweza kunitishia maisha kweli hadi nimsahau Mngu kiasi hiki, hadi nishindwe kusali? Hadi nishindwe kwenda kanisani? Usikute ni kajani kameletwa tu na upepo, alfu unahama nyumba, chunguza udhaifu wa hicho kitu, utaona kwamba kinaanza kwa mikwara kama Antiokus lakini mwishowe kumbe ni hafifu kabisa, hakina kitu.
Hivyo, vitu kama ugonjwa, umaskini, ada za shule, zisikutishe ufikiri kana kwamba ati Mungu hayupo, au uone ati hivyo vimekuwa vya muhimu kuliko Mungu. Ukivichunguza utagundua kwamba hivyo ni vitu vidogo tu.Acha kuogopeshwa na maneno ya watu unashindwa kumtegemea Mungu. Tambua daima Mungu anashinda tu.
©️ Pd. Prosper Kessy OFMCap.